Swahili | English

MAKALA ZA ELIMU

FAHAMU KUHUSU POMBE.

Angalizo; Tunapoongelea kuhusu pombe sio kwamba tunahamasisha kutumia pombe bali tuelewe kile tunachofanya kwa mapenzi ya Mungu! pombe haikukataliwa ila itumike kwa kiasi.

Mhubiri 9:7
Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.

Tito2:3
Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;

1 Timotheo 5:21-23
"21 Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.
23. Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.

Yoshua Bin Sira 31:25-29
"25. Usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa pombe, maana imewaangamiza wengi.26 Tanuru hupima ugumu wa chuma, na pombe hupima mioyo katika shindano la wenye kiburi. 27. Pombe ni kama uhai kwa mtu akinywa kwa kiasi, Maisha yafaa nini bila pombe? Imeumbwa iwafurahishe watu.28. Kunywa pombe kwa wakati wake na kwa kiasi, kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.29. Lakini kunywa pombe kupita kiasi, kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha."

Wakolosai 2:16-18a
"Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika VYAKULA au VINYWAJI,au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.18.Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake..."

Luka 7:31-35
"31 Yesu akaendelea kusema, "Basi, nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani? 32 Ni kamavijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine: 'Tumewapigieni ngoma lakini hamkucheza! Tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!'33 Kwa maana Yohane alikuja, akawa anafunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: 'Amepagawa na pepo!'.34 Naye mwana wa Mtu amekuja anakula na kunywa, nanyi mkasema: 'Mwangalieni mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi!'35 Hata hivyo, hekima ya Mungu imethibitishwa kuwa njema na wote wale wanaoikubali."

#Note; mvinyo itumike kwa kiasi, kama huwezi kutumia kwa kiasi, ni afadhali kuacha kabisa.

Prayer

Kipanda uso ni nini...?

Ni ugonjwa au maumivu makali ya kichwa yanayo weza kuuma sehemu yeyote ya kichwa na kusababisha na mwingiliano wa homoni, mishipa ya damu na ya fahamu.

Dkt Kigocha Okeng'o Daktari Bingwa wa Mishipa ya Fahamu Ubongo na Misuli Mloganzila

Health

Sheria

Kuelewa sheria huwasaidia watu binafsi kuendesha haki na wajibu wao.

Usalama

Usalama unahusisha kuwalinda watu binafsi na jamii kutokana na madhara, ikiwa ni pamoja na usalama wa kimwili, usalama wa mtandao na kujiandaa kwa dharura.

MASWALI NA MAJIBU

Bofya swali ili kuona jibu.

JE, SHERIA YA MAPADRE KUTOOA NA KUISHI USEJA IMEANDIKWA WAPI KATIKA BIBLIA AU IMETUNGWA TU NA PAPA?

Mtu anapouliza kila kitu kimeandikwa wapi katika Biblia ni kudhihirisha kutokuijua au kuilewa vizuri Biblia Takatifu na historia yake. Mtu anapong'ang'ania "nionyeshe kitu fulani kimeandikwa wapi kwenye Biblia" ni kutaka kujiona ya kwamba yeye anailewa sana Biblia na ameisoma yote kwa hiyo kila kitu kilichopo kwenye Biblia anakifahamu kumbe haijui Biblia bali anakariri Biblia!

Na hili suala la kushupalia swala la kuoa linadhihirisha jinsi gani tulivyo kizazi cha zinaa, ni kama tunadhani kuwa UZIMA upo katika kujamiana! La hasha.

Paulo anasema "Kwa sababu ya zinaa ni bora kuoa na kuolewa" (1 Wakoritho 7:2-9) haya sio maneno ya kufurahia na kuchekelea tu maana "YANAWALENGA WALE WALIOSHINDIKANA KATIKA YALE YAPENDEZAYO"(1 Wakorintho 7:1-8) sasa ni lazima tujiulize je tumeshindikana kiasi hicho?, hiyo sio sifa!

1 Wakorintho 7:1-8
"Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo"

Na Paulo Mtume anasema "Ni bora kuoa au kuolewa" lakini hakusema "Ni LAZIMA kuoa au kuolewa"

Suala la kutooa kwa mapandre kadiri ya historia lilianza tangu zamani kabisa mwanzoni mwa milenia ya pili katika mtagusi wa pili wa Laterani mwaka wa 1139 ili waweze kumtumikia Mungu kwa uhuru na bila mawaaa wala pasipo vikwazo(1 Wakorintho 7:32-35)

1 Wakorintho 7:32-35
"32.Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya Bwana ampendezeje Bwana;33.bali yeye aliyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendeza mkewe.34-Tena iko tofauti kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili apate kuwa Mtakatifu mwili na Roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.,35. Nasema hayo niwafaidie ninyi, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine"

Watu wengine wanafikiri kwamba kutooa ni dhambi, kama ni hivyo basi hata Yesu mwenyewe alikosa maana hata yeye mwenyewe hakuoa. Yesu mwenyewe anafundisha kuhusu ubikira (Mathayo 19: 10-12)

Mathayo 19:10-12,
"Wanafunzi wake wakamwambia, kama mambo ya mme na mke yakuwa hivyo ni afadhali kutuooa kabisa. Lakini Yeye akawaambia 'SI WOTE WAWEZAO KULIPOKEA NENO HILO, ILA TU WALE WALIOJALIWA, maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi, tena wako Matowashi WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWA AJILI YA UFALME WA MBINGUNI", awezaye kulipokea neno hili na alipokee"

Yesu mwenyewe analifafanua jambo hili kwa mapana, katika orodha ya matowashi Yesu aliowataja, Mapadre ni Matowashi waliojifanya hivyo kwa ajili ya huduma ya kanisa na ufalme wa Mungu.

Tena Yesu anatuambia waziwazi kwamba" sio wote wawezao kulipokea neno hilo" yaani sasa sio wote wawezao kuwa Matowashi (Mapadre) bali ni wale tu waliojaliwa na Mungu neema hiyo. Wale wasioweza kuishi upadre huoa na kuwa na familia. Tena Yesu anamalizia kwa kusema " Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee", kwa maana nyingine ni kusema "Fundisho au Utowashi huu sio wa lazima" anayeweza kuishi maisha hayo basi na ayapokee na yule asiyeweza basi aache!

Vilevile Mitume ili kumfuata Yesu kikamilifu waliyaacha yote waliokuwa nayo ikiwepo familia zao ili wamtumikie Bwana (Mathayo 19:27-29)

Mathayo 19:27-29:
"Ndipo Petro akajibu akamwambia 'Tazama sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe, tutapata nini basi?,29. Amini nawaambia, kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu wa kiume au wakike, au baba au mama au watoto au mashamba KWA AJILI YA JINA LANGU, atapokea mara mia zaidi na kuurithi uzima wa milele" katika injili hiyo, Yesu anadhihirisha kwamba aliyeacha hayo yaliotajwa si kwa sababu hawezi kuyapata la hasha, bali ameyaacha hayo yote KWA AJILI YA JINA LA YESU atapokea mengi hapa duniani halafu tena ataurithi ufalme wa mbinguni.

Mapadre wameyaacha hayo yote , wameacha nyumba, familia zao na kila kitu SIO KWA SABABU HAWANA UWEZO AU HAWAWEZI KUPATA MAMBO HAYO bali WAMEACHA KWA SABABU YA KUMTUMIKIA MUNGU KWA KADIRI YA MAANDIKO MATAKATIFU na kwakutaka kwao kuyaishi kikamilifu MASHAURI YA INJILI ikiwepo USEJA.

Maneno ya Mtume Paulo na yale ya Yesu mwenyewe kuhusu kumtumikia Mungu bila kuoa sio ya bahati mbaya bali ndiyo njia bora na inayofaa sana na kukubalika mbele ya Mungu. Kwa hiyo unapowaona mapadre hawaoi ujue sababu yake ni hiyo kwamba "Wamejitoa kwa ajili ya kulihudumia Kanisa"

(Na pia huwa nawashangaa mno watu wanaowapiga vita Mapadre kwamba kwa nini hawaoi, najiuliza je, hao Mapadre wamewakataza wao kwamba wasioe?.)..na kama jibu ni hapana, sasa Je,"Pilipili ya shamba usiyoila inakuwashia nini?"

Kwa nini Wakatoliki husali kwa watakatifu?

Wakatoliki huwaomba watakatifu wawaombee, kama tunavyowaomba marafiki watuombee. Watakatifu wako karibu na Mungu mbinguni.

Je! ni nini umuhimu wa Rozari?

Rozari ni sala ya kutafakari ambayo husaidia Wakatoliki kutafakari matukio muhimu katika maisha ya Yesu na Maria.