UANACHAMA KWA MUJIBU WA KATIBA:
Kuna aina tatu za uanachama.
Wanachama washiriki
Awe kijana Mkatoliki mwenye umri kati ya miaka 14 hadi 17.
Wanachama kamili
- Kijana Mkatoliki mwenye Ubatizo.
- Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 35.
- Awe mwenye Akili timamu.
- Awe na Mapenzi na VIWAWA.
- Vijana ambao wameowa na kuolewa pia wanaweza kuwa wanachama na viongozi.
Wanachama maalumu
- Aliyekwisha kuwa mwanachama kamili.
- Watu wa wazima wenye mapenzi mema na chama.
Wajibu wa Mwanachama.
- Kukubali kuongozwa na Mwongozo wa chama na kutekeleza malengo yake.
- Kushiriki mikutano ya chama kwa mujibu wa KATIBA.
- Kushiriki shughuli zote za VIWAWA.
- Kushiriki katika chaguzi mbalimbali za VIWAWA.
- Kulipa ada na michango maalum kwa wakati unaotakiwa.
- Ada ya mwanachama shirikishi 1000 TZS kwa mwezi na Ada ya mwanachama kamili 2000 TZS.
- Kuunga mkono na kusaidia kwa vitendo maendeleo ya VIWAWA.
- Kusikiliza na kufuata maelekezo mbalimbali ya Uongozi.
Haki za Mwanachama
- Anahaki ya kuchagua au kuchaguliwa kwa mujibu wa ibara namba (7.1,2) na (9.2) ya KATIBA.
- Kuchangia hoja na kusikilizwa katika mikutano kwa nidhamu.
- Kushiriki shughuli zote za VIWAWA kwa mujibu wa KATIBA.
- Anahaki ya kupata huduma, faida zitokanazo na chama kwa mujibu wa taratibu za chama mahalia.
- Mwanachama maalumu hawezi kuchagua au kuchaguliwa katika Uongozi.
- Mwanachama maalumu hawezi kufanya maamuzi kwa niaba ya Kamati Tendaji.
- Mwanachama anapotuhumiwa anahaki ya kupewa fursa za kujieleza,kujitetea.
Ukomo wa Mwanachama
- Akikiuka maadili ya chama kama kushiriki katika kuihujumu VIWAWA.
- Kufariki dunia.
- Kuvuka kikomo cha umri wa miaka 35.
- Hiari ya mwanachama ambayo itadhibitishwa na Uongozi.